Alhamisi 30 Aprili 2026 - 03:30
Ujerumani: Iran imeidhalilisha Marekani

Hawza/ Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz alisema: Donald Trump aliihukumu vibaya Tehran na sasa hana mkakati wowote wenye ufanisi dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz aliikosoa vikali Washington na akaonya kwamba; serikali ya Marekani imekuwa ikitumiwa vibaya na watu wasio na uwezo, na “imedhalilishwa” na Tehran, na kwa sasa haina mkakati wazi wa kumaliza migogoro yake.

Merz, akiwa katika ziara ya shule moja katika eneo lake la kuzaliwa magharibi mwa Ujerumani, alisema: Marekani iliitathmini vibaya mfumo wa Iran na ikaingia katika vita bila kuwa na mpango sahihi wa kutoka katika mgogoro huo.

Aliongeza kuwa: Wairani ni wenye nguvu zaidi kuliko ilivyotarajiwa waziwazi, na Wamarekani hawana mkakati wa kuridhisha katika mazungumzo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ujerumani likimnukuu: “Marekani yote imedhalilishwa na uongozi wa Iran.”

Merz amekuwa mara kadhaa akionya kuhusu athari za kiuchumi za vita na nchi yoyote, hasa Iran, na siku ya Jumatatu alisisitiza tena kwamba: “Vita hivi vina gharama kubwa sana kwetu.”

Chanzo: POLITICO

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha